Home kimataifa KUMBE! WACHEZAJI SPURS WALITOROKA KAMBI ENGLAND

KUMBE! WACHEZAJI SPURS WALITOROKA KAMBI ENGLAND


 WACHEZAJI wawili wa timu ya taifa ya Argentina ambao wanacheza ndani ya kikosi cha Tottenham Spurs watapigwa faini kwa kosa la kutoroka kambini na kujiunga na timu yao ya taifa bila kupewa ruhusu maalumu ambao ni Cristian Romero na Giovani Lo Celso.

Imeelezwa kuwa wachezaji hao wawili walitoroka nchini England na kwenda kujiunga na kambi ya timu ya taifa ya Argentina ambayo ilikuwa inamenyana na Brazil katika kuwania kufuzu Kombe la Dunia ila ulifutwa na utapangiwa tarehe nyingine.

Mchezo huo uliyeyuka katika dakika ya sita baada ya maafisa wa Wizara ya Afya ya Brazil kuingia uwanjani na kuwatoa wachezaji hao ambao walitakiwa kukaa karantini kwa muda kabla ya kucheza mchezo huo kwa ajili ya tahadhari dhidi ya Corona.

Spurs wamesema kuwa watawachukulia hatua wachezaji hao kwa kuwa waliondoka katika timu hiyo bila kufuata utaratibu ikiwa ina maana kwamba jamaa walitoroka kambini.

Nyota mwingine ambaye alitoroka ni pamoja na Davinson Sanchez yeye alisepa na kujiunga na timu yake ya taifa ya Colombia, sasa wachezaji hao watatakiwa kukaa karantini kwa muda wa siku 10 nchini Croatia kabla hawajarejea kwenye timu zao kukutana na rungu linalowasubiri.

SOMA NA HII  MERIDIANBET KASINO INAKULETEA MCHEZO WA MAOKOTO COBRA QUEEN.