Home news SIMBA: HAIKUWA BAHATI YETU,WACHEZAJI WALIPAMBANA

SIMBA: HAIKUWA BAHATI YETU,WACHEZAJI WALIPAMBANA


BAADA ya mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara, Simba kubanwa mbavu mbele ya Biashara United wamebainisha kuwa walipambana kusaka ushindi ila haikuwa bahati yao.

Katika mchezo wa kwanza wa msimu wa 2021/22 uliochezwa Uwanja wa Karume,Mara, mbele ya mashabiki wengi waliojitokeza ubao ulisoma Biashara United 0-0 Simba.

Unakuwa ni mwanzo wa kipekee kwa Simba ambao msimu wa 2020/21 mchezo wao wa kwanza walishinda kwa mabao 2-1 mbele ya Ihefu ambayo kwa sasa inashiriki Championship ila jana Septemba 28 waligawana pointi mojamoja na Biashara United.

Seleman Matola, Kocha Msaidizi wa Simba amesema kuwa haikuwa bahati yao kushinda licha ya kupambana kusaka ushindi.

“Haikuwa bahati yetu, wachezaji walipambana kwa namna ambavyo wanaweza lakini tumeshindwa kushinda, matokeo tunayachukua tutafanya kazi mchezo ujao kwani ligi inaanza na kila timu inahitaji ushindi,”.

Kituo kinachofuata kwa Simba ni dhidi ya Dodoma Jiji inayonolewa na mzawa Mbwana Makata. 

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Oktoba Mosi, Uwanja wa Jamhuri, Dodoma.

Ikiwa imetoka kulazimisha sare na kugawana pointi moja inakutana na Dodoma Jiji iliyotoma kuwanyoosha Ruvu Shooting bao 1-0 Uwanja wa Jamhuri, Dodoma.

SOMA NA HII  KISA ISHU YA BWALYA KUKOSA PENATI JUZI...PABLO ASHINDWA KUJIZUIA SIMBA...ACHUKUA UAMUZI MGUMU...