Home news UZI MPYA WA SIMBA 2021/22 HUU HAPA

UZI MPYA WA SIMBA 2021/22 HUU HAPA


 KLABU ya Simba imeweka wazi kuwa kwa sasa jezi mpya kwa msimu wa 2021/22 zinapatikana kwenye maduka yote ya Vunja Bei.

Ezekiel Kwamwaga, Kaimu Ofisa Habari wa Simba amesema kuwa kutokana na maombi ya mashabiki wengi wa Simba kuzihitaji jezi hizo wakaona hakuna tatizo wakaamua kuziruhusu zipatikane madukani.

“Awali ilikuwa tumepanga kuzindua rasmi Septemba 4 kutokana na maombi ya mashabiki wengi wa Simba tumeamua kuziruhusu kupatikana katika maduka ya Vunja Bei.


“Ni jezi nzuri na bora na kila shabiki ajivunie na apate jezi yake orijino nina amini kwamba hakuna ambaye ataweza kupenda kuona anavaa kitu feki hilo halipo hivyo kila mmoja ajipatie jezi mpya.

“Kuhusu uzinduzi siku ya Jumamosi bado upo palepale na tutatoa utaratibu namna mambo yatakavyokuwa ni suala la kusubiri na kuona,” .

SOMA NA HII  FT: DODOMA JIJI 0-1 SIMBA SC....BALEKE AANZA KUJIBU MASWALI MAGUMU...SAWADOGO MHH..