Home news TAMBWE:LIGI DARAJA LA KWANZA NI NGUMU KWELIKWELI

TAMBWE:LIGI DARAJA LA KWANZA NI NGUMU KWELIKWELI


AMISS Tambwe, mshambuliaji wa timu ya DTB inayoshiriki Championship amesema kuwa ligi hiyo ni ngumu kwa kuwa kila timu inapambana kufanya vizuri.

Mchezo wake wa kwanza nyota huyo raia wa Burundi aliweza kufunga mabao maane na kuweka rekodi ya kuwa mshambuliaji wa kwanza kufunga hat trick ilikuwa mbele ya African Lyon. 

Katika mchezo mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Uhuru dakika 90 zilikamilika na ubao ulisoma DTB 4-1 African Lyon.

Tambwe aliyafunga mabao hayo dakika ya 12, 40, 46 na 54, huku lile la African Lyon likifungwa dakika ya 80 kupitia kwa Wilbart Mkimbu.


Mchezaji huyo ambaye amewahi kucheza Simba na Yanga kwa nyakati tofauti amesema:”Ligi Daraja la Kwanza ni ngumu kwa kuwa kila timu inapambana ili kufika juu.

“Haina tatizo kwa namna ambavyo tumejipanga tuna amini kwamba tutafanya vizuri na kila mchezaji anajua kazi yake ni katika kutimiza majukumu,” amesema.

SOMA NA HII  WANACHOKITAKA MASTAA YANGA NI HIKI HAPA MBALI NA MKWANJA