MATAIFA matatu ilibidi yaungane kutengeneza bao la kwanza kwa Simba kwa msimu wa 2021/22, kutokana na kuwa kwenye wakati mgumu katika mechi tatu mfululizo ambazo walicheza.
Ikumbukwe kwamba Simba inayonolewa na Kocha Mkuu Didier Gomes ilinyooshwa na watani zao wa jadi Yanga Septemba 25 kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii kwa kichapo cha bao 1-0 ikiwa imetoka kunyooshwa pia bao 1-0 dhidi ya TP Mazembe kwenye mchezo wa kirafiki.
Ilikuwa kwenye mchezo wa Simba Day, siku ya utambulisho wa wachezaji na benchi la ufundi kwa mashabiki Simba pia ilipoteza Uwanja wa Mkapa.
Aliyepeleka kilio kwa Simba katika mchezo wa Ngao ya Jamii anaitwa Fiston Mayele ambaye alimtungua kipa namba moja wa Simba, Aishi Manula kwa pasi ya mshikaji wake Farid Mussa.
Kwenye mchezo wa kwanza wa ligi mbele ya Biashara United pia ililazimisha sare ya bila kufungana na kufanya wagawane pointi mojamoja.
Mchezo huo ulichezwa Uwanja wa Karume, Mara kwa wale wanaojiita Wanajeshi wa Mpakani.
Iliibuka Uwanja wa Jamhuri, Dodoma baada ya ushindi wa bao 1-0 baada ya mataifa matatu kuungana ili kupata bao hilo na kazi ilianza kwa kipa Aishi Manula yeye ni Mtanzania kisha Chris Mugalu huyu ni raia wa Congo alitoa pasi na mtupiaji alikuwa Meddie Kagere huyu ni raia wa Rwanda.
Ikiwa imecheza mechi mbili za ligi ikiwa imekusanya pointi nne na kuyeyusha pointi mbili kati ya sita ambazo ilikuwa inazisaka.