News

MBEYA KWANZA KUANZA MAZOEZI KESHO

admin October 6, 2021 5:43 pm


KESHO Oktoba 7 kikosi cha Mbeya Kwanza kinatarajiwa kuanza mazoezi kwa ajili ya maandalizi ya Ligi Kuu Bara.

Timu hiyo imeanza vizuri mechi za awali ambapo mchezo wake wa kwanza ilishinda mbele ya Mtibwa Sugar bao 1-0 na ililazimisha sare ya kufungana mabao 2-2 dhidi ya Mbeya Kwanza.

Katika mchezo wa Dabi ya Mbeya ushindani ulikuwa mkubwa na Mbeya Kwanza walipindua meza kibabe na kufanya ubao kusoma Mbeya City 2-2 Mbeya Kwanza.

Mabao yote ya Mbeya Kwanza yalifungwa na Crispian Ngushi ambaye alifunga bao bora kwa mzunguko wa pili kwa mtindo wa Acrobatic.

Taarifa rasmi kutoka Mbeya Kwanza imeeleza kuwa kesho kikosi kinatarajiwa kuanza mazoezi baada ya wachezaji kupewa mapumziko ya muda wa siku tatu.


 

ORODHA YA WACHEZAJI WA SIMBA WALIOANZA MAZOEZI LEO BOKO KOCHA YANGA AKIRI KUWA KUNA TATIZO KWENYE SAFU YA USHAMBULIAJI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply