Ligi Kuu

RASMI LIGI KUU BARA KUITWA NBC PREMIER LEAGUE

admin October 6, 2021 10:43 am


LEO Oktoba 6 Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania, (TFF) limemtambulisha Mdhamini Mkuu wa Ligi Kuu Tanzania Bara ambaye ni beki ya NBC.

Sasa ni rasmi Ligi Kuu Tanzania itafahamika kwa jina la NBC Premier League baada ya kusaini mkataba na TFF wenye thamani ya bilioni 2.5.

Ni Rais wa TFF, Wallace Karia amesaini dili hilo na Mkurugenzi wa NBC Theobald Sabi naye alisaini kwa upande wa NBC.

Kwa sasa Ligi Kuu Bara itakuwa inaitwa NBC Premier League kwa kuwa ni wadhamini wakuu.

Karia amesema kuwa miongoni mwa mchanganuo wa fedha hizo ni pamoja na kuutumia kwenye usafiri.

“Wakati wadhamini wa kwanza wanaingia wa ligi kuu madhumuni makubwa ilikuwa ni kusaidia usafiri wa timu kwenda kituo kingine kucheza mechi zake na hakukuwa na tatizo tena la timu kushindwa kufika kwenye kituo kwa sababu za kushindwa kumudu gharama za usafiri.

“Sisi kama TFF hatujabadili kitu sehemu kubwa ya hela hii itakwenda kwenye klabu kwa ajili ya kuwa sehemu ya usafiri sehemu ya mshahara tayari ishakuwa Coverd,”.

DUH ETI BARCELONA HATA IKICHEZA MASAA MATATU HAIWEZI KUFUNGA NENO KUTOKA KWA RAIS WA TFF, KARIA BAADA YA KUPATA UDHAMINI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply