kimataifa

DUH ETI BARCELONA HATA IKICHEZA MASAA MATATU HAIWEZI KUFUNGA

admin October 6, 2021 10:43 am


 BEKI wa Barcelona, Gerard Pique amesema kuwa timu yao inaweza kucheza kwa masaa matatu uwanjani na bado ikashindwa kufunga bao.

Barcelona imekuwa ikionyesha kiwango cha chini sana kwenye Ligi Kuu ya Hispania msimu huu ikiwa imepoteza mchezo wake wa kwanza Jumapili.

Timu hiyo imefanikiwa kushinda michezo mitatu tu kati ya saba ambayo wamecheza hadi sasa kwenye Ligi Kuu Hispania msimu huu. 

Jumapili, Barcelona walilala kwa mabao 2-0 dhidi ya Atletico Madrid mchezo ambao walionyesha kiwango kibovu sana.

Pique ambaye alionekana kuzungumza kwa hasira na mchezaji mwenzake Sergio Busquets, amesema hawawezi kufunga bao hata kama watacheza kwa masaa matatu uwanjani.

 Barca sasa wapo kwenye nafasi ya tisa kwenye wakiwa pointi tano nyuma ya Atletico Madrid ambao wamecheza michezo michache zaidi.

“Tulikuwa vizuri na tulionyesha kiwango cha juu sana, lakini ukweli ni kwamba bado tunatatizo kubwa kwenye eneo la ushambuliaji.

 “Tumefungwa mabao mawili rahisi sana, na kila mmoja anaweza kuona hilo, sina shaka na kila kinachoendelea lakini ukweli ni kwamba tunaweza kucheza hata masaa matatu bila kufunga bao lolote,” alisema Pique ambaye ni mchezaji mkongwe zaidi kwenye timu hiyo.


KOCHA TWIGA STARS AWAZUNGUZMIA WAPINZANI WAKE RASMI LIGI KUU BARA KUITWA NBC PREMIER LEAGUE

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply