Burudani

M-BET YAMWAGA SH MILIONI 961 KWA WASHINDI, SHABIKI WA YANGA KUTOKA NJOMBE ASHINDA SH 104.3

admin October 7, 2021 12:43 pm


KAMPUNI ya mchezo ya kubashiri ya M-Bet Tanzania imetumia jumla ya Sh. milioni 961 kuwazawadia washindi mbalimbali wanaobashiri kwa usahihi matokeo ya ligi mbalimbali duniani kupitia mchezo wa Perfect 12 na Jackpot Bonus .

Hayo yalisemwa na Meneja Masoko wa kampuni ya M-Bet Tanzania, Allen Mushi wakati wa kumzawadia zawadi yake Stephano Ndunguru kutoka mkoani Njombe aliyeshinda Sh104.3 millioni.

Mushi alisema kuwa Ndunduru anakuwa mshindi wa 10 kuzawadiwa mamilioni ya fedha kwa mwaka huu na kuifanya kampuni yao kutumia kiasi hicho cha fedha.

 Alisema kuwa wanajisikia faraja sana kuendelea kubadili na kuwawezesha wanamichezo kupitia michezo yao ya kubashiri na sasa kuwa na maisha bora.

“Mbali ya kubadili maisha ya washindi wetu kupitia kubashiri michezo, pia tunajisikia fahari kuchangia  asilimia 20 ya kodi ya ushindi ambayo inaigia moja kwa moja Serikalini . Sisi ni walipa kodi wazuri wa Serikali na tunachangia maendeleo,” amesema Mushi.

Ameongeza kuwa kati ya fedha hizo, Sh791millioni ni zawadi za moja kwa moja kwa washindi wakati Sh200 millioni ni zawadi kwa ya ‘jackpot’ bonus. 

Ameongeza kuwa wanatarajia kuwazadia washindi wengi  mwaka huu kwani ligi mbalimbali zinaendelea mpaka sasa.

Kwa upande wake, Ndunduru ambaye ni shabiki wa Yanga amesema kuwa hakuamini kushinda kiasi hicho cha fedha kwa kutumia Sh1,000 tu. “Mimi mkulima wa maharage, nimekuwa nikibashiri na kupata hela ndogo ndogo. Nilipopigiwa simu na kuambiwa kuwa nimeshinda zaidi ya milioni 100, sikuamini  na nilidhani ni ndoto,” amesema Ndunduru.

Amesema kuwa fedha hizo atazitumia kuendesha kilimo cha kisasa zaidi na kutoa ajira kwa watu.

NDEGE MPYA YA AZAM FC INAYOTEMBEA ARDHINI KUPITA KWA MWENDO WA TARATIBU KWA SASA NI ZAMU YA STARS, ACHA KAZI IENDELEE

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply