Azam FC

NDEGE MPYA YA AZAM FC INAYOTEMBEA ARDHINI KUPITA KWA MWENDO WA TARATIBU

admin October 7, 2021 10:43 am


MENEJA Masoko na Mauzo wa Azam FC, Tunga Ally, leo Alhamisi Oktoba 7 ameongoza zoezi la makabidhiano ya basi jipya la Azam FC ambalo wao wanaita ndege ya ardhini.

Gari hilo matata na bora ni Mercedes Benz Irizar i6S Plus ambapo makabidhiano yamefanyika kwa dereva mpya atakayeendesha basi hilo (mwenye bluu) mpaka Dar es Salaam. 

Dereva aliyelitoa basi hilo nchini Afrika Kusini, alimkabidhi funguo dereva mpya, kwa ajili ya kuanza safari ya kuwasili jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Azam FC, Zakaria Thabit amesema kuwa ndiga hiyo itakuwa katika mwendo wa kawaida ili kuwaruhusu mashabiki wa Azam FC kuweza kuliona basi hilo.

Dereva ambaye amekabidhiwa basi hilo ataendelea na safari ya kuibuka Dar  kupitia miji ya Mbeya, Iringa na Morogoro.

Tunga pia aliwakabidhi madereva wote jezi mpya za Azam FC zenye ubora mkubwa wa kimataifa.

CHEKI NAMNA WACHEZAJI WA SIMBA WALIVYOKUWA WAKIKIMBIZANA M-BET YAMWAGA SH MILIONI 961 KWA WASHINDI, SHABIKI WA YANGA KUTOKA NJOMBE ASHINDA SH 104.3

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply