News

SIMBA YALIA NA ISHU YA VIWANJA KUSHINDWA KUWA RAFIKI KWAO

admin October 7, 2021 6:43 am


 BAADA ya kukamilisha dakika 180 za msako wa pointi sita ndani ya Ligi Kuu Bara na kuambulia nne, mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara, Simba wamebainisha kuwa ubovu wa viwanja umewanyima uhuru wa kucheza mpira wa pasi nyingi waliouzoea.

Kikosi hicho kilifungua pazia la ligi kwa kucheza na Biashara United kwenye Uwanja wa Karume, Mara na kushindwa kufungana, kabla ya mchezo wa pili dhidi ya Dodoma Jiji pale Uwanja wa Jamhuri, Dodoma, kuibuka na ushindi wa bao 1-0.

Akizungumza na Spoti Xtra, Kocha Msaidizi wa Simba, Seleman Matola, alisema: “Ninaweza kusema kwamba ligi ina ushindani mkubwa na kila timu inahitaji ushindi, hilo ni jambo zuri, lakini kwetu tulianza kwa tabu kidogo hasa ukizingatia sehemu ya kuchezea haikuwa rafiki kwetu.

“Ukitazama wachezaji wetu wamepambana sana kusaka ushindi ila ilikuwa ni ngumu kucheza ule mchezo ambao tumeuzoea wa pasi pamoja na kuwapa uhuru wachezaji kushinda mapema, hakuna namna lazima mapambano yaendelee,” .

Mfungaji wa bao la kwanza kwa Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes alikuwa ni Meddie Kagere alipachika bao hilo Uwanja wa Jamhuri,Dodoma.

Alifunga bao hilo akiwa ndani ya 18 kwa shuti la mguu wake wa kulia akitumia pasi ya mshambuliaji mwenzanke, Chris Mugalu.

GOMES APIGA HESABU KUHUSU WAPINZANI WAKE,MASHABIKI WAMZUNGUKA KIBADENI AGUSIA ISHU YA CHAMA NA LUIS,AIONYA SIMBA KUHUSU YANGA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply