Home news KIUNGO MPYA SIMBA APEWA PROGRAM MAALUMU KWA AJILI YA WABOTSWANA

KIUNGO MPYA SIMBA APEWA PROGRAM MAALUMU KWA AJILI YA WABOTSWANA


 KIUNGO mshambuliaji wa Simba, Pape Ousmane Sakho, amepewa programu maalum na benchi la ufundi la timu hiyo, ili kuhakikisha anakuwa fiti mapema kwa ajili ya michezo ijayo hususani wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Jwaneng Galaxy ya Botswana.

Sakho alipata majeraha ya kifundo cha mguu kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara ambao Simba waliibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Dodoma Jiji.

Oktoba 17, mwaka huu, Simba itakuwa Botswana kucheza dhidi ya Jwaneng Galaxy, mechi ya mkondo wa kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya kwanza.

Akizungumza na Spoti Xtra, Meneja wa Simba, Patrick Rweyemamu, alisema: β€œSehemu ya kikosi chetu ambayo haipo kweΒ­nye majukumu ya timu za taifa kwa sasa inaendelea na mazoezi katika Uwanja wa Boko Veterani, ili kujiweka sawa kwa ajili ya michezo yetu ijayo ya Ligi Kuu Bara na Ligi ya Mabingwa Afrika.

β€œKuhusiana na hali ya majeruhi mpaka sasa hakuna majeruhi yeyote, kwani hata Pape Ousmane Sakho ambaye alikuwa na majeraha tayari ameanza kufanya programu maalum ya mazoezi kwa ajili ya kuongeza spidi uponaji wa jeraha lake.”


SOMA NA HII  WAKATI KIBU DENIS AKIMIMINIWA MAMILIONI TENA...WASAIDIZI WAPYA WA MBRAZILI SIMBA WATAJWA..