Namungo FC

LUSAJO ANAIWINDA HESABU YA BOCCO

admin October 11, 2021 2:43 pm


 KINARA wa chati ya wafungaji bora kwenye Ligi Kuu Bara mpaka sasa, Reliants Lusajo amefunguka kuwa malengo yake makubwa ni kuhakikisha anafunga mabao mengi zaidi msimu huu ili kutimiza ndoto yake ya kutwaa kiatu cha ufungaji bora ambacho kinatetewa na nahodha wa Simba John Bocco.

Lusajo katika michezo miwili iliyopita ya Namungo amefanikiwa kufunga mabao mawili, akifunga bao moja kwenye mchezo dhidi ya Kagera Sugar na mchezo dhidi ya Geita Gold. 

Mshambuliaji huyo msimu wa 2019/20, akiwa na kikosi cha Namungo alifanikiwa kuibuka mfungaji bora namba nne naada ya kufunga mabao 12.

Akizungumza na Championi Jumatatu, Lusajo alisema: “Kama kikosi tumekuwa na mwanzo mzuri wa msimu huu ambapo mpaka sasa hatujapoteza mchezo wowote katika michezo yetu miwili ya kwanza, lakini nafurahi pia kuanza vizuri kwa kufunga mabao mawili katika michezo hiyo.

“Malengo ya kila mshambuliaji ni kuhakikisha anafunga mabao, hivyo natumaini nitaendelea kuwa katika kiwango bora kama ilivyo sasa, na kufunga mabao mengi ili kutimiza malengo yangu ya kushinda tuzo ya mfungaji bora.”

MAJEMBE YA KAZI YAANZA KUKIWASHA SIMBA JADON SANCHO MAMBO MAGUMU NDANI YA MANCHESTER UNITED

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply