news

MAJEMBE YA KAZI YAANZA KUKIWASHA SIMBA

admin October 11, 2021 2:43 pm


 WACHEZAJI wa Simba ambao walikuwa wanasumbuliwa na majeraha tayari wamerudi uwanjani kuendelea na mazoezi kuwawinda Jwaneng Galaxy ya Botswana.


Majembe hayo ya kazi yamekuwa na mwendelezo mzuri ndani ya kikosi hicho na pale wanapopata nafasi wamekuwa wakifanya kazi nzuri kutimiza majukumu yao.

Ni Erasto Nyoni ambaye ni beki pamoja na Shomari Kapombe hawa walipata majeraha kwenye mechi za Ligi Kuu Bara na kushindwa kuendelea na majukumu yao.


Ikumbukwe kwamba wawili hawa waliitwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars ila walipewa muda wa mapumziko kwa kuwa hawakuwa fiti.

Kwa upande mwingine kiungo wa kazi chafu, Mzamiru Yassin naye pia amejumuika kwenye kikosi kinachonolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes katika mazoezi yaliyofanyika Uwanja wa Boko Veteran, Bunju.

Pia Simba ilikuwa na mchezo wa kirafiki leo wa mazoezi ya ndani ilikuwa dhidi ya Cambiasso inayonolewa na Kocha Mkuu, Mecky Maxime na ilikamilika kwa sare ya kufungana bao 1-1.

SAKHO AZUNGUMZA KISWAHILI AKIWA NA MSHIKAJI WAKE WAWA LUSAJO ANAIWINDA HESABU YA BOCCO

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply