KOCHA Msaidizi wa Azam FC, Vivier Bahati, ameelezea mipango yao ya kuwamaliza Pyramids ya nchini Misri.
Azam itacheza mchezo huo wa raundi ya kwanza ya Kombe la Shirikisho Afrika wakiwa nyumbani katika viwanja vya Azam Complex Chamanzi nje kidogo ya Jiji la Dar, leo Jumamosi.
Kuelekea mchezo huo wa raundi ya kwanza Azam imeanza kutesti mitambo kwa kucheza mchezo wa kirafiki na KMC na kuwafunga 3-2 wikiendi iliyopita.
Mabao yote matatu ya Azam yalisababishwa na mshambuliaji wao Ayoub Lyanga huku akitoa asisti kwa Idris Mbombo na Daniel Amoah, na kona ambayo KMC walijifunga.
Akizungumza na Championi Ijumaa, Bahati amesema kuwa: “Mchezo wetu na KMC ilikuwa kutizama maandalizi tuliyoyafanya kuelekea mchezo wetu na Pyramids na tunaona vijana wamekaa