news

KISA TAIFA STARS..MANULA APEWA SHAVU LA UHAKIKA SIMBA..GOMES AFUNGUKA A-Z

admin October 16, 2021 1:00 am


KOCHA Mkuu wa Simba, Didier Gomes, amesema itakuwa ngumu kumuweka benchi kipa Aishi Manula ndani ya kikosi chake kutokana na ubora ambao anazidi kuuonesha kila siku.

Ndani ya kikosi cha Simba, Manula anaunda safu ya makipa sambamba na Beno Kakolanya, Jeremiah Kisubi na Ally Salim.

Akizungumza na Soka la Bongo, Gomes alisema: “Manula ni golikipa mzuri, kwa sasa ni miongoni mwa magolikipa bora ndani ya Afrika, anajiamini na anazidi kuimarika kila siku.

“Nimemtazama akiwa na kikosi cha timu ya taifa, alikuwa bora sana na aliisaidia timu yake kushinda.

“Ndani ya Simba ni ngumu kumuweka benchi, yeye atabaki kuwa kipa namba moja wa timu lakini bado kuna nafasi ya makipa wengine kupata nafasi katika kikosi chetu. Yupo Kakolanya, Kisubi na Salim, wote wanazidi kuimarika kila siku.”

KWA UMAFIA HUU WA SIMBA..HAO WABOTSWANA WANAKUFA MAPEMA TU..CORONA YAHUSISHWA KISA MECHI NA KMC….YANGA WAINGIA ‘BARIDI’ WABADILI GIA ANGANI..ISHU NZIMA IKO HIVI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply