News

SIMBA YAWAFANYIA ‘DANGANYA TOTO’ WABOTSWANA…WAFIKIA HOTELI YA KITAJIRI ZAIDI

admin October 16, 2021 4:00 pm


SIMBA wajanja sana kimataifa. Kumbe juzi buana walitanguliza wachezaji wanne Botswana kama chambo ili kuwavuruga Jwaneng Galaxy.

Jamaa wakajaa wakajua ndiyo imewasili kumbe ndiyo kwaanza majembe yapo Boko yanajinoa. Gazeti la Mwanaspoti limeripoti kwamba Ibrahim Ajib, Gadiel Michael, Ally Salim na Jimmyson Mwanuke walitangulia na viongozi kama kuzuga tu na kuwachanganya wapinzani.

Viongozi wawili wa Simba, Mohamed Nassoro na Crescentius Magori ndio waliokuwa wamefika Botswana kuweka mambo sawa sambamba na mratibu Abbas Ally. Kikosi cha Simba, kilifikia katika hoteli ya Avan iliyopo Gaborone ambayo inasifika kwa utulivu wa hali ya juu, usalama na ufahari ambapo gharama kwa kila chumba ni Dola 110 sawa na Sh250,000.

Mmoja wa viongozi wa Simba aliiambia Mwanaspoti kwamba wamechukua tahadhari kubwa kwenye mechi hiyo ndani na nje ya uwanja.

AZAM FC vs PYRAMIDS NGOMA BADO MBICHI…KIGONYA AWA SHUJAAA BAADA YA SIMBA KUPIGA TIZI LA KWANZA BOTSWANA..GOMES AFUNGUKA HAYA..ATAJA IMANI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply