1: GREAT WIN Mnyama .. 2 away Goals.. Clean Sheet Safi.. Well Done Mnyama! 🦁 Vile ndivyo Timu kubwa Afrika hufanya katika hatua za awali za Ligi ya Mabingwa.
2: Unawakumbuka Al Ahly katika hatua za awali? Hucheza kimkakati, sio burudani. Tumia nafasi haraka iwezekanavyo kisha shusha kasi ya mchezo, tunza nguvu zako.. Safari bado ndefu!
2: Approach safi kwa benchi la ufundi la Simba👏 Ni wazi walifanya tafiti ya kutosha kuijua Galaxy! Licha ya kuwa na vimo vya kutisha, lakini Galaxy wana matatizo makubwa kwenye Utimamu wa mwili. Kiufundi wakafaidika, kivipi?
4: Ligi ya Bostwana imesimama kwa miezi 18 sasa! Licha ya kufanya mazoezi Afrika Kusini, Match Fitness ilikuwa tatizo kwa Galaxy. Simba wakawalazimisha mapema kugombea mipira ya juu kwenye boksi lao.. Wakapata nafasi na kuzitumia kikatili.
5: Aishi Manula👏 What A Perfomance! One of The Best Goal Keeper katika bara la Afrika hivi sasa! Ni mtulivu mguuni, hesabu nzuri kwenye kucheza krosi.. Akili yake ilitumika zaidi leo kuliko mikono yake.
6: Galaxy walijitahidi kucheza soka la pasi fupi lakini wakapata changamoto ya spidi. Simba waliblock vyema njia za mipira na kuwafanya Galaxy wachezee mpira katika eneo lisilokuwa na madhara.
7: Sio bahati mbaya Henock Inonga kuwa beki bora wa Ligi ya Congo msimu uliopita✊ Ana maarifa makubwa kwenye kuhesabu mikimbio ya mshambuliaji anapovamia lango lake! Pasi yake ya kwanza kwa viungo inarahisisha ‘build up’ ya shambulizi.
8: Morrison angekuwa ‘siriaz’ kidogo, Simba wangeweza kupata bao kutoka mguuni mwake! Alijiweka kwenye maeneo sahihi lakini alikosa maamuzi sahihi.
9: Galaxy walikamia sana, pumzi ikawa kisoda..Matokeo yake wakacheza sana kwa mdomo na refa kuliko kupanga mipango yao.
10: Well done Bocco👏 Well Done Kanoute.. A Modern Box To Box ! Mtulivu na anafika haraka kwenye kila tukio katikati ya kiwanja.
Nb: Simba ni ileile.. kilichopungua ni Kelele tu 😂