Azam FC

BAADA YA KUNUSA HALI YA HATARI…LWANDAMINA AWAITA CHAPCHAP MASTAA WAKE KAMBINI

admin October 19, 2021 1:00 pm


KOCHA Mkuu wa Azam FC, George Lwandamina,amekirejesha kikosi chake kambini haraka baada ya kuwapa mapumziko ya siku moja.

Wikiendi iliyopita Azam ilitoka suluhu na Pyramid ya Misri kwenye mchezo wao wa hatua ya kwanza ya Kombe la Shrikisho Afrika.

Azam itacheza na Biashara United octoba 19 katika Uwanja wa Benjamini Mkapa nje kidogo ya Jiji la Dar, huku huo ukiwa mchezo wao wa tatu wa Ligi.

Ofisa Habari wa Azam, Thabiti Zakaria amesema kuwa kocha wao amewataka wachezaji wote kufika kambini haraka.

“Mwalimu amewataka wachezaji warudi kambini kesho (leo), kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa Ligi Kuu na Biashara na baadaye mchezo wa marudiano na Pyramid, nafikiri anataka kuona wanajiandaa vyema kabla ya michezo hiyo,” alisema Zaka.

KUHUSU WANAOM’BEZA KUWA HATAIWEZA NAFASI YA CHAMA…BWALYA AWAJIBU HIVI MOURINHO NA ‘SIZITAKI MBICHI HIZI’ KUHUSU KULA SHAVU LA UKOCHA WA NEWCASTLE UNITED

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply