News

IKIWA NA POINTI TISA KIBINDONI….KIKOSI CHA YANGA CHATUA DAR KIBOSI…

admin October 20, 2021 9:08 am


KIKOSI cha Yanga kimetua saa 4:00 asubuhi hii kikitokea Songea mkoani Ruvuma kwenye mchezo wa ligi dhidi ya KMC na kuunganisha moja kwa moja kuhani msiba wa mchezaji mwenzao.

Yanga jana walikuwa ugenini dhidi ya KMC kwenye uwanja wa Majimaji na kufanikiwa kupata ushindi wa bao 2-0 ukiwa ni mchezo wao wa tatu kukusanya pointi zote tatu baada ya Kagera Sugar kuifunga bao 1-0 na Geita Gold bao 1-0.

Kaimu Mtendaji Mkuu wa Yanga, Senzo Mazingiza anasema wanashukuru kupata pointi tisa kwenye michezo yote waliyocheza na wanaahidi kuendeleza ushindi kwenye michezo iliyombele yao.

“Msimu uliopita ni kweli tulianza vizuri lakini tukashindwa kuwa na mwendelezo mzuri msimu huu kikosi chetu ni bora na kinabadirika kadri siku na mechi zinavyochezwa hivyo hatutarajii kurudia yaliyopita,” anasema.

Akizungumzia kwenda kuhani msiba Temeke alisema mchezaji Paul Godfrey ‘Boxer’ ameondokewa na mzazi wake hivyo kama familia wameona umuhimun wa kwenda kumpa pole na kumsindikiza mzazi wao kwenye nyumba ya milele.

“Boxer ni Yanga amepata shida hatuwezi kumuacha peke yake kwenye kipindi hiki kigumu anachokipitia ni jambo jema tukaungana naye ili kumfariji,” anasema.

BAADA YA KUIAZIBU JWANENGA YA BOTSWANA..SIMBA YAENDELEA KUWA GUMZO AFRIKA…YAIFUNIKA AL AHLY BAADA YA KUIRARUA KMC…YANGA WAITANGAZIA VITA AZAM FC..SENZO AWEKA MIPANGO HADHARANI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply