Home news HUKU SAIDO AKIWA HAJUI HATMA YAKE YANGA…KAZE IBUKA NA HILI KUHUSU MAYELE..AMTAJA...

HUKU SAIDO AKIWA HAJUI HATMA YAKE YANGA…KAZE IBUKA NA HILI KUHUSU MAYELE..AMTAJA FEI TOTO


BAADA ya Yanga kupata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya KMC, Kocha Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi ametamka kuwa hivi sasa anaanza kuona mabadiliko ya timu yake ikianza kucheza kwa kuelewana.

Juzi Jumanne, Yanga iliibuka na ushindi huo katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa kwenye Uwanja wa Majimaji mkoani Songea.

Katika mchezo huo, mabao ya Yanga yalifungwa na mshambuliaji Mkongomani, Fiston Mayele dakika ya 5 na kiungo Feisal Salum ‘Fei Toto’ dakika ya 12.

Akizungumza kwa niaba ya Nabi, Kocha Msaidizi wa Yanga, Mrundi, Cedric Kaze, alisema kuwa mabadiliko yameanza kuonekana katika mchezo huo baada ya kuona wachezaji wakicheza kwa kuelewana, huku wakifuata maelekezo yao.

Kaze alisema kuwa safu ya kiungo na ushambuliaji inacheza kwa kuelewana kwa kupigiana pasi nzuri za kufunga mabao huku wakitumia pembeni kuanzisha mashambulizi ambayo yamewapa matokeo mazuri.

Aliongeza kuwa, licha ya kuona mabadiliko, bado hawajafikia kile kiwango wanachokitaka kwa kucheza soka safi la kuvutia na idadi kubwa ya mabao.“Nafurahi kuona timu yetu imeanza kuelewana, bado sijaifikia Yanga ile ninayoitaka, naamini bado kidogo nitaipata, kikubwa mashabiki wawe na subira.

“Katika mchezo wetu dhidi ya KMC timu ilionekana kuwa na mabadiliko baada ya kucheza vile ambavyo tumewapa maelekezo wachezaji wetu na kufanikiwa kupata ushindi huo wa mabao 2-0.“

Katika kipindi cha pili, wachezaji wetu walicheza kwa maelekezo yetu makocha kwa kuwaacha wapinzani wachezee mpira katika eneo lao, tukiamini wataingia kwa kubadilika na kushambulia kwa spidi na siyo kwamba vijana wetu waliishiwa pumzi,” alisema Kaze

SOMA NA HII  KIEMBA AFUNGUKA KILICHOWAPONZA SIMBA