News

ALICHOKISEMA MWIJAKU KUHUSU KUTEMBEA UCHI BAADA YA SIMBA KUFUNGWA JUZI…

admin October 26, 2021 10:00 am


MHAMASISHAJI wa Klabu ya Simba, Mwijaku  amegoma kufanya kile alichoahidi hivi karibuni kwa mashabi wa Simba mbele ya waandishi wa habari, baada ya kutoa kauli yake ya kwamba angetembea utupu bila nguo, endapo Simba ingepoteza katika mchezo wa marudiano wa klabu bingwa Afrika dhidi ya Jwaneng Galaxy ya Botswana.

Mwijaku amedai kwamba alikua tayari kutekeleleza ahadi yake lakini amejua kwamba sheria ya nchi haimruhusu kufanya hivyo.

Ikumbukwe klabu ya Simba imeondoshwa katika Ligi ya Mabingwa Afrika kwa msimu huu na Jwaneng Galaxy ya Botswana baada ya kuruhusu kufungwa bao 3-1 nyumbani kwenye mchezo wa juzi jumapili katika dimba la Benjamin Mkapa.

Hayo yanajiri baada ya Simba kuruhusu kufungwa mabao matatu nyumbani na kufanya uwiano wa mabao kuwa 3-3 baada ya kushinda 2-0 ugenini hivyo wameondolewa kwa kanuni ya bao la ugenini.

WAKATI SIMBA WAKIITAJA YANGA KIPIGO LIGI YA MABINGWA..MANARA AJIBU MAPIGO… BREAKING :..GOMES ATUPIWA VIRAGO MSIMBAZI…MRITHI WAKE ATAJWA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply