News

BREAKING :..GOMES ATUPIWA VIRAGO MSIMBAZI…MRITHI WAKE ATAJWA

admin October 26, 2021 10:14 am


Klabu ya Simba imesema imeridhia ombi la aliyekuwa Kocha Mkuu, Didier Gomes da Rosa la kuachana na Simba kuanzia leo Oktoba 26, 2021.

Simba kupitia mtandao wao wamesema baada ya tathmini na majadiano ya kina, pande zote zimeafikiana kwa mujibu wa mkataba na manufaa ya wote.

Wamesema kutokana na hatua hiyo, aliyekuwa Kocha Msaidizi Thierry Hitimana, ndiye atakuwa Kocha Mkuu wa Simba katika kipindi hiki cha mpito akisaidiwa na Selemani Matola.

Aidha, Klabu pia imefanya mabadiliko madogo katika benchi la ufundi kwa kusitisha mikataba ya aliyekuwa Kocha wa Makipa, Milton Nienov na Kocha wa Viungo, Adel Zrane.

ALICHOKISEMA MWIJAKU KUHUSU KUTEMBEA UCHI BAADA YA SIMBA KUFUNGWA JUZI… BAADA YA KIMYA KIREFU….MWAKALEBELA AIBUKA NA JIPYA NDANI YA YANGA…ATAJA HUJUMA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply