News

WAKATI SIMBA WAKIKIPIGA LEO…MCHEZAJI WAO AIBUKA NA KUIPA YANGA UBINGWA MSIMU HUU

admin October 27, 2021 6:00 am


NYOTA wa zamani wa klabu ya Simba raia wa Ghana Nicholas Gyan amesema kuwa Yanga ya msimu huu ni bora kuliko Yanga zote za misimu minne iliyopita na ina nafasi ya kutwaa ubingwa.

Gyan alisema Simba hawatakiwi kubweteka badala yake wawe makini kwa kuwa mwenendo wa Yanga ya msimu huu unaonekana bora sana na kila mchezo wanaocheza wanaonekana kubadilika na kuwa bora zaidi.

Gyan ambaye kwa sasa yupo na kikosi cha DTB FC kinachoshiriki Ligi Daraja la Kwanza, aliwahi kutwaa mataji mawili akiwa na Simba, msimu wa 2017-18 na 2018-19 kisha akatemwa baada ya kukosa nafasi ya kudumu.

Akizungumza na Championi Jumatatu Gyan alisema: “Uwa natazama mechi ya Simba na Yanga kama ambavyo imekuwa desturi ya Watanzania wengi. Yanga wanaonekana kuwa wanahitaji kitu msimu huu.

“Na kwa namna ambavyo walivyo bora naona wanakwenda kufanya mambo makubwa sana, siyo Yanga ile ya misimu minne nyuma, hii iko bora zaidi na Simba wanatakiwa kuwa makini zaidi kwa kuwa mwisho wanaweza kutoka kapa.”

BAADA YA KUANZA KUFUNGA FUNGA SANA….’FEI TOTO’ AJIPA MAZIMA UFALME WA YANGA BAADA YA TAARIFA ZA KUPEWA RUSHWA NA WALIBYA KUWA NYINGI..BIASHARA UTD WAIBUKA NA HILI…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply