Msemaji wa klabu ya Young Africans Haji Manara ametaja sababu za kikosi cha Simba SC kupoteza mchezo wa Jumapili (Oktoba 24), dhidi ya Jwaneng Galaxy ya Botswana.
Simba SC ilipoteza mchezo huo wa Mkondo wa Pili wa Ligi ya Mabingwa Barani Afrika kwa mabao 3-1, na kujikuta ikitupwa nje ya michuano hiyo.
Manara ametaja sababu ambazo anaamini zilichangia Simba SC kupoteza kirahisi mchezo huo, alipohojiwa Wasafi FM mapema jana Jumatano (Oktoba 27).
Manara amesema: “Simba Sc walitolewa klabu Bingwa Afrika kutokana na Dharau Mchezaji Kama Morrison walikua wanapanda mpira wakati timu inahitaji Ushindi Mimi Binafsi naumizwa na timu za Tanzania kufanya vibaya katika mashindano ya kimataifa”
“Tulitolewa kwenye Ligi ya Mabingwa barani Afrika kwasababu ya Pre Season yetu haikuwa nzuri, lakini kadri siku zinavyozidi kwenda timu inazidi kuwa bora”
“Nakuhakikishia kama Rivers Utd tungekuwa tunacheza nao kipindi hiki wangekula tano”
“Tumetolewa na River United ya Nigeria kwa bahati Mbaya Leo hii wale River United wakija kwa mkapa leo wanapigwa Goli tano”
“Hatuna matatizo ndani ya klabu ya Yanga Sc, Kocha Nabi hana Matatizo na wachezaji wetu kila kitu kipo sawa Yanga Sc ipo vizuri katika mahusiano na wachezaji wake”
“Msimu huu Yanga na Azam zina vikosi bora zaidi ya Simba, ukiangalia sisi Yanga tumesajili wachezaji kama Khalid Aucho, Fiston Mayele, Yannick Bangala, Heritier Makambo, Djuma Shaban ambao wote wameingia kikosi cha kwanza kama ilivyo Azam lakini Simba wachezaji wao wapya wengi wanakaa benchi,”
“Ukitaka kujua muunganiko wetu umetimia waulize tuliokutana nao, sisi tunapiga pasi 60 kwenye mechi moja haina shida, tunatengeneza nafasi, watu wanasema tunatengeneza nafasi nyingi hatufungi magoli mengi ‘magoli yatakuja tu’ ukitaka kujua ubora wa timu lazima utengeneze nafasi…
“Nasema na narudia kuna siku mtu atajaa kwenye 18 ya Young Africans (@yangasc ) atakula 9, zile nafasi tunazotengeneza kuna siku mtu atakula 9, kila nafasi goli.”