Home news PAMOJA NA KUANZA KUICHEZEA YANGA..AUCHO ASHINDWA KUKAA KIMYA.. AFUNGUKA HAYA..ATAJA UBORA..

PAMOJA NA KUANZA KUICHEZEA YANGA..AUCHO ASHINDWA KUKAA KIMYA.. AFUNGUKA HAYA..ATAJA UBORA..

 


YANGA inatamba na mashine nyingi mpya, lakini kuna jina moja linatajwa mpaka kwa watani zao, Simba, ambalo ni la kiungo Khalid Aucho.

Lakini, kama unadhani jamaa ameanza kazi ndani ya klabu hiyo, basi sahau ametamka kauli itakayowashtua hata Azam ambao watakutana nao wikiendi hii.

Akizungumza na  Gazeti la Mwanaspoti, Aucho ambaye kazi yake katika mechi tatu imepeleka ujumbe kwamba ni kiungo wa kazi ametamka kwamba kama unapima kazi yake ndani ya Yanga basi ni mapema kufanya hivyo na kwamba ile kubwa bado hajaianza.

“Mbona bado sijaanza kazi. Hapa ni mapema sana kwangu, nashukuru tu nimeanza vyema, lakini sijaanza kuonyesha ule ubora wangu ambao ninaoujua. Naweza kusema bado nipo katika utangulizi sana wa kiwango changu,”alisema nahodha huyo msaidizi wa Uganda Cranes.

Kiungo huyo aliongeza kwamba anachoomba tu kwa sasa ni kuendelea kufanya kazi yake bila kuumia na kama hilo litafanikiwa, basi kuna ubora mkubwa ambao mashabiki wa Yanga watachekelea uwepo wake katika timu hiyo.

Diara ukutani

Akizungumzia ubora wa Yanga kutoruhusu bao mpaka sasa, kiungo huyo anayevaa jezi namba 8 alisema ishu sio kuwa na mabeki bora, lakini inatokana na kikosi chao kuwa na kipa bora, Diarra Djigui.

Aucho alisema wakati mabeki na viungo wakabaji wakifanya vizuri kuna ubora mkubwa wa Diara ambao unasimama juu ya kazi zao.

“Sio kwamba Yanga ina mabeki bora sana, lakini siku zote ubora wa kazi yetu na viungo, inatokana na ubora wa kipa tuliyenaye. Hapa Yanga tuna kipa bora sana Diarra ambaye amethibitisha ubora wake. Lakini kifupi tuna makipa bora kwa sababu hata hawa wengine Ramadhan (Kabwili) na Eric (Johola) nao wamekuwa bora sana.”

Akimzungumzia Aucho, kipa wa zamani wa Yanga, Benjamin Haule alisema ni kiungo anayejituma vyema kusaidiana na mabeki kukaba, wakati mwingine husaidia mashambulizi.

“Aucho ni kiungo mahiri na anajua kitu gani anakihitaji akiwa uwanjani. Yupo makini, anajua ni wakati gani wa kuuficha mpira mguuni, kuzuia na kushambulia wakati mwingine,” alisema.

SOMA NA HII  SIMBA HAKUNA KUPOA, WAPITILIZA KAMA UTANI

Kwa upande wa staa wa zamani wa timu hiyo, Said Bahanunzi alisema ubora wa Aucho utaongeza ushindani dhidi ya Mukoko Tonombe, Zawadi Mauya na Yanick Bangala.

“Aucho ni kiungo bora katika nafasi ya ukabaji. Hiyo itaimarisha safu hiyo, kwani tayari wapo kina Mukoko ambao ni mafundi,” alisema.