MCHEZO wa Ligi Kuu Bara kati ya wenyeji Simba na Coastal Union kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa umemalizika kwa kwa Suluhu (0-0).
Kipindi cha kwanza kilimalizika kwa Suluhu (0-0) licha ya kwamba kila timu ilijitahidi kuonesha jitihada za kupata bao la kuongoza ndani ya dakika 45 za kwanza lakini ikashindikana.
Katika kipibdi cha kwanza Simba ililazimika kufanya mabadiliko ya lazima baada ya Sadio Kanoute na Muzamiru Yassin kuumia kwa pamoja baada ya kugongana na wachezaji wanne wa Coastal katikati ya kiwanja na nafasi zao kuchukuliwa na Jonas Mkude na Benard Morrison.
Jacoeb Benedicto wa Coastal Union ndiye mchezaji pekee aliyeoneshwa kadi ya njano katika dakika 45 za kipindi cha kwanza baada ya kumchezea faulo, Kanoute dakika ya 17.
Kipindi cha pili kilirejea kwa wenyeji Simba kulishambulia lango la Coastal mara kwa mara lakini baadi ya wachezaji wake akiwemo John Bocco, Kibu Denis na Mohamed Hussein hawakutumia nafasi kwa ufasaha.
Issa bushehe na Hija Ogando wa Castal Union waliingia Uwanjani dakika ya 57 baada kuchukua nafasi za wachezaji wawili waliotoka na dakika moja baadae Simba ilimtoa Hassan Dilunga na nafasi yake kuchukuliwa na Yusuph Mhilu.
Dakika ya 72 Benedicto wa Coastal alioneshwa kadi ya pili ya njano kisha nyekundu baada ya kudharau maamuzi ya mwamuzi katika pigo la mpira wa kutenga la Simba na Coastal kusalia uwanjani na wachezaji 10.
Dakika ya 78 Simba ilifanya mabadiliko kwa kumtoa Mohamed Hussein na kuingia Meddie kagere ambaye aliingia kuongeza nguvu kwenye safu ya ushamhuliaji ya timu yake.
Simba iliendelea kutafuta bao na dakika ya 80 hadi 90 ililishambulia lango la Coastal mfululizo lakini jitihada zao hazikuzaa matunda na katika dakika za nyongeza beki wa Simba Henoc Inonga alioneshwa kadi nyekundu ya moja kwa moja baada ya kumchezea faulo mchezaji wa Coastal na mechi kumalizika kwa Suluhu.