Home news BREAKING :..GOMES ATUPIWA VIRAGO MSIMBAZI…MRITHI WAKE ATAJWA

BREAKING :..GOMES ATUPIWA VIRAGO MSIMBAZI…MRITHI WAKE ATAJWA


Klabu ya Simba imesema imeridhia ombi la aliyekuwa Kocha Mkuu, Didier Gomes da Rosa la kuachana na Simba kuanzia leo Oktoba 26, 2021.

Simba kupitia mtandao wao wamesema baada ya tathmini na majadiano ya kina, pande zote zimeafikiana kwa mujibu wa mkataba na manufaa ya wote.

Wamesema kutokana na hatua hiyo, aliyekuwa Kocha Msaidizi Thierry Hitimana, ndiye atakuwa Kocha Mkuu wa Simba katika kipindi hiki cha mpito akisaidiwa na Selemani Matola.

Aidha, Klabu pia imefanya mabadiliko madogo katika benchi la ufundi kwa kusitisha mikataba ya aliyekuwa Kocha wa Makipa, Milton Nienov na Kocha wa Viungo, Adel Zrane.

SOMA NA HII  #CAFCCUPDATES: KAPOMBE AZIBA PENGO LA MORRISON SIMBA...KIKOSI KAMILI HIKI HAPA...