Home Uncategorized KOCHA KATWILA AIPIGA BONGE MOJA YA MKWARA NAMUNGO

KOCHA KATWILA AIPIGA BONGE MOJA YA MKWARA NAMUNGO

 


BAADA ya kupoteza mchezo dhidi ya Azam FC kwa kufungwa mabao 2-0, Ihefu leo Jumamosi watakuwa wenyeji wa Namungo FC, Uwanja wa Sokoine.

 

 Huu unakuwa mchezo wa pili kwa kocha Zubeir Katwila kuiongoza timu hiyo ambayo imekuwa na matokeo mabaya kwenye ligi.

 

 Akizungumza na Championi Jumamosi, kocha huyo amesema wameyafanyia kazi makosa yaliyojitokeza kwenye mchezo dhidi ya Azam FC na anaamini watafanya vyema kwenye mchezo huo.

“Makosa yale yaliyosababisha tufungwe kwenye mchezo dhidi ya Azam tumeyafanyia kazi na tunaimani kubwa kuwa mchezo wetu dhidi ya Namungo tutafanya vizuri” alisema.

 

Mpaka sasa Ihefu wamecheza michezo saba na kufanikiwa kupata pointi tatu huku wakiwa kwenye nafasi ya pili kutoka mwisho kwenye msimamo wenye timu 18.

 

SOMA NA HII  KOCHA STARS:TUNAKWENDA KUPINDUA MEZA KIBABE KENYA