Home Uncategorized RASMI SIMBA KUWEKA KAMBI MAREKANI

RASMI SIMBA KUWEKA KAMBI MAREKANI


KOCHA Mkuu wa Simba, Patrick Aussems, raia wa Ubelgiji na mwekezaji wa timu hiyo, mfanyabiashara Mohammed Dewji wamekubaliana kwa pamoja kuipeleka timu hiyo nchini Marekani katika kambi ya maandalizi ya msimu ujao.

Aussems amekubaliana hivyo na Mo baada ya kufanikiwa kutetea ubingwa wa Ligi Kuu Bara. Na amefunguka hivyo katika mahojiano yake Jumatatu kwenye Hoteli ya Sea Scape jijini Dar jana.

Ikumbukwe kuwa huu ni msimu wa pili kwa timu hiyo kwenda kuweka kambi nje ya nchi baada ya mwanzoni mwa msimu huu kwenda Uturuki katika kambi ambayo imewapatia mafanikio makubwa.

Aussems alisema kuwa tayari wameshakubaliana na Mo kuwa kambi ya maandalizi ya msimu ujao itafanyika katika nchi ya Marekani inayoongozwa na Rais Donald Trump.

“Maaandalizi ya msimu ujao tutaanza baada ya kukamilisha ligi ambayo Jumanne (kesho) ndiyo itakuwa inafikia mwisho baada ya kupewa kombe letu, kwa sababu tuna mengi ya kufanya ikiwemo suala la maandalizi ya kambi ya maandalizi kwa msimu ujao.

“Lakini tumeshakubaliana na jana nilikuwa na Mo mwenyewe kuongelea suala hilo wapi tutaweka kambi japokuwa uongozi wao walitaka zaidi twende tukaweke kambi nchini Ureno lakini nimemueleza Mo kwamba ni vyema tukaenda kuweka kambi nchini Marekani, jambo ambalo ameshalipitisha, hivyo kwangu nasubiria wakati uweze kufika,” alisema Aussems.

SOMA NA HII  POGBA AWATUMIA UJUMBE WALIOTAKA AACHWE NDANI YA MANCHESTER UNITED