Home news FARID MUSSA AFUNGUKIA PACHA YAKE NA MAYELE

FARID MUSSA AFUNGUKIA PACHA YAKE NA MAYELE


 KIUNGO Mshambuliaji wa Yanga, Farid Mussa ambaye ameonekana kuelewana vizuri na mshambuliaji wa timu hiyo, Fiston Mayele, amefunguka kwamba, pacha yao msimu huu itatisha sana.

Farid katika mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Simba uliochezwa Septemba 25, mwaka huu kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar, alitoa asisti kwa Mayele ambaye alifunga bao pekee lililowapa ushindi wa 1-0.

Ilikuwa ni pasi ya kwanza kwa kiungo huyo kwa msimu mpya wa 2021/22 na iliwapa furaha mashabiki wa Yanga kwa kuwa walisepa na taji la Ngao ya Jamii mbele ya watani zao wa jadi Simba.

Akizungumza na Spoti Xtra, Farid amesema kuwa: “Kombinesheni yangu na Fiston ipo vizuri, nina imani tutafanya mengi mazuri msimu huu, japo timu nyingi zinazokutana na Yanga huwa zinatupania sana,”.

Farid amekuwa na mwendelezo mzuri kwenye mechi za Ligi Kuu Bara ambapo aliweza kuaminiwa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi kuweza kuanza kikosi cha kwanza.

Yanga imecheza mechi mbili za ligi ambapo ile ya ufunguzi ilikuwa Uwanja wa Kaitaba na Yanga ilishinda kwa bao 1-0 na mchezo wa pili ulichezwa Uwanja wa Mkapa, Yanga ilishinda bao 1-0 dhidi ya Geita Gold.


SOMA NA HII  SKUDU,KONKON NA YANGA KUNA KITU HAKIPO SAWA HAPA