Home news IMEFICHUKA..KUMBE KOCHA HITIMANA ALIFUNGUKA HAYA KABLA YA KUCHEZA NA WABOTSWANA

IMEFICHUKA..KUMBE KOCHA HITIMANA ALIFUNGUKA HAYA KABLA YA KUCHEZA NA WABOTSWANA


KOCHA msaidizi wa Simba Hitimana Thiery amesema kuwa watarudi kwa nguvu zote kuhakikisha kuwa wanafanya vizuri katika michezo ya ligi kuu mara baada ya kumaliza ratiba yao ya michuano ya ligi ya Mabingwa.

Simba mpaka sasa katika michezo ya ligi kuu imefanikiwa kucheza michezo miwili pekee dhidi ya Biashara United na Dodoma Jiji ambapo wamefanikiwa kushinda katika mchezo mmoja na kutoa sare mmoja jumla wakiwa na pointi 4.

Akizungumza na Championi Jumatatu, Hitimana Thiery alisema kuwa watu wasifikiri kuwa wamewekeza nguvu katika michuano ya kimataifa pekee kwani malengo yao ni kuhakikisha wanafanya vyema katika kila michuano wanayoshirki na baada ya kumaliza kwa ratiba ya michuano hiyo wataelekeza nguvu zote katika michezo ya ligi kuu.

“Kila michuano ambayo Simba inashiriki malengo ni kufanya vizuri, hivyo watu wasifikiri kuwa labda tumewekeza nguvu katika michuano ya kimataifa pekee hapana hata kwenye michezo ya ligi kuu tutahakikisha kuwa tunafanya vizuri.

“Malengo ya Simba katika ligi kuu yapo wazi ni kuhakikisha kuwa tunatetea ubingwa ambao tuliweza kuubeba msimu uliopita, hivyo tutarejea kwa kishindo na kufanya vizuri katika michezo yetu ijayo ya ligi ili tuweze kuendelea kufanya vizuri na kuwa ndani ya malengo yetu ambayo hayawezi kutimia kama hatushindi,”alisema kocha huyo.

SOMA NA HII  BAADA YA TAMBO ZA YANGA KUPITIA KWA MANARA KUWA NYINGI...KIGOGO SIMBA AFUNGUKA HAYA