Home Ligi Kuu JINSI USHINDI WA SIMBA SC DHIDI YA POLISI TZ ULIVYOISAIDIA YANGA LEO…

JINSI USHINDI WA SIMBA SC DHIDI YA POLISI TZ ULIVYOISAIDIA YANGA LEO…


BAO la dakika ya 90 lililofungwa kwa mkwaju wa penalti na Rally Bwalya lilitosha kuwapa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Polisi Tanzania.

Penalti ya Simba imetokea baada ya beki wa Polisi Tanzania kumchezea vibaya Bernard Morrison ndani ya box.

Kwa matokeo hayo yanaifanya Simba ifikishe pointi saba baada ya kushinda michexo miwili na kutoka sare ya bila kufungana na Biashara walipata matokeo dhidi ya Dodoma Jiji na Polisi leo ambao wanashuka nafasi ya pili wakiipisha Yanga wanaopanda kwa utofauti wa mabao.

Dakika 30 za kipindi cha kwanza kulikuwa wazi kwa Simba kupata bao, baada ya kufika mara kwa mara, langoni mwa Polisi Tanzania, ila safu yao ya mbele ilikosa utulivu.

Simba walitumia mfumo wa 4-3-3 ambapo mbele walikuwa Rally Bwalya, Meddie Kagere na walikuwa wanasaidiwa na Kibu Denis na Hassan Dilunga waliokuwa anatokea pembeni.

Pamoja na kwamba washambuliaji hao walikuwa wanafika ndani ya 18 ya Polisi Tanzania, umakini wa mabeki Kelvin Yondani na Juma Makapu walikuwa wanaondosha mipira ya hatari kwa uharaka.

Kwa upande wa Polisi Tanzania ni kama walifanya mashambulizi ya kushitukiza, lakini walijikuta wanakosa mipango ya kumalizia mipira kwenda langoni kwa kipa Aishi Manula.

Dakika 41 Polisi Tanzania walilishambulia lango la Simba ambapo walikuwa wanapigiana pasi, zilizowapa presha mabeki wa Wanamsimbazi.

DAKIKA 45 ZA KIPINDI CHA PILI

Kocha wa Simba, Thiery Hitimana alifanya mabadiliko dakika ya 46, alimtoa Kibu na nafasi yake ilizibwa na Bernard Morrison ambaye alichangamsha safu yao ya mbele.

Dakika ya 56 Simba ilipiga shuti lililolenga langoni kwa Metacha kupitia kwa Dilunga aliyepiga shuti Kali ambalo likaokolewa.

Kipindi cha pili kilikuwa cha wazi kwa kila timu kufika langoni kwa mpinzani, kutokana na kucheza kwa kufunguka na kushambuliana kwa zamu.

Dakika ya 63 kocha wa Polisi Tanzania, Hamsini Malale alimtoa Adam Adam na alimuingiza Kassim Shaban.

Wakati kwa upande wa Simba ilifanya mabadiliko dakika ya 69 alitoka Nyoni/Mzamiru Yassin, Kagere/John Bocco.

SOMA NA HII  KWA MFUMO HUU MPYA WA SIMBA....YANGA MJINDAE KUFUNGWA MENGI AISEE...

Dakika ya 90 Juma Ramadhan alilimwa kadi nyekundu baada ya kumchezea rafu, Morrison na Simba ikapewa penalti, iliyopigwa na Rally Bwalya na ikazaa bao