Home kimataifa LUKAKU NA ZLATAN YAWAKUTA, WAPIGWA PINI ITALIA

LUKAKU NA ZLATAN YAWAKUTA, WAPIGWA PINI ITALIA


 KAMATI ya nidhamu ya Ligi Kuu ya Italia imewafungia mastaa wawili kwenye ligi hiyo, Zlatan Ibrahimovic wa AC Milan na Romelu Lukaku wa Inter Milan.

Hatua hiyo imefikia baada ya mastaa hao kukorofishana kwenye mchezo wa robo fainali ya Copa Italia, Jumanne ya wiki hii wakati Inter Milan ikishinda mabao 2-1.

Chama cha soka cha Italia kimewafungia wachezaji hao ambao walitaka kukinukisha ndani ya uwanja mara mbili kwenye mchezo wa michuano hiyo.

Pia adhabu hiyo ni tofauti na ile ambayo Zlatan alipewa uwanjani baada ya kuonyeshwa kadi nyekundu kwa kuwa alionyeshwa jumla ya kadi mbili za njano.

Lukaku ambaye alionyeshwa kadi ya njano ataukosa mchezo wa nusu fainali ya kwanza dhidi ya Juventus huku chama hicho kikiweka wazi kwamba bado hakijapitia taarifa ya mwamuzi na kama kutakuwa na makosa mengine basi adhabu hiyo inaweza kuongezeka. 

SOMA NA HII  BAADA YA USHINDI JANA NA KUINGIA NNE BORA EPL...ARTETA AANZA TAMBO ...AJIKUTA NAYE NI 'BAB KUBWA'..