Home CAF RAJA CASABLANCA MABINGWA WA KOMBE LA SHIRIKISHO CAF

RAJA CASABLANCA MABINGWA WA KOMBE LA SHIRIKISHO CAF


 KLABU ya Raja Casablanca ya nchini Morocco, imetwaa Kombe la Shirikisho Afrika baada ya ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya JS Kabylie ya Algeria usiku wa kuamkia leo huko jijini Cotonou nchini Cameroon.

 

Mabao ya Raja yalifungwa na washambuliaji wake, Soufiane Rahimi dakika ya 5 na Mkongomani Ben Malango Ngita dakika ya 14, kabla ya Mohammed Zakaria Boulahia kuifungia Kabylie bao la kufutia machozi dakika ya 46.

 

Baada ya Shirikisho sasa, Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika itafuatia Jumamosi ijayo ambayo itazikutanisha Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini na mabingwa watetezi, Al Ahly ya Misri kwenye Uwanja wa Mohamed V Jijini Casablanca, Morocco.


Timu hizo mbili ambazo zimetinga hatua ya fainali zilikutana na Simba ya Tanzania kwa nyakati tofauti.


Al Ahly ilikuwa ni kwenye hatua ya makundi ambao Simba ilishinda mchezo mmoja na ilipoteza mchezo mmoja huku Kaizer Chiefs ilikutana na Simba kwenye robo fainali na mchezo wa kwanza Simba ilifungwa mabao 4-0 ugenini na ule wa pili Simba ilishinda mabao 3-0 ila iliishia hatua hiyo kwa idadi ndogo ya mabao.

SOMA NA HII  KOMBE LA SHIRIKISHO: NAMUNGO 0-0 NKANA FC