Home news KIMEUMANA YANGA…AUCHO, BANGALA WAZUA BALAA JIPYA…MUKOKO AAMUA KUFUNGUKA A-Z

KIMEUMANA YANGA…AUCHO, BANGALA WAZUA BALAA JIPYA…MUKOKO AAMUA KUFUNGUKA A-Z


MCHEZAJI Bora wa Yanga msimu uliopita, Mukoko Tonombe amekiangalia kikosi cha sasa na kukiri wazi Khalid Aucho na Yannick Bangala ni balaa jipya kwenye soka la Bongo na kwamba hata yeye analazimika kukuna kichwa ili arejee kikosi cha kwanza.

Mukoko bado hajafanikiwa kucheza hata dakika moja katika msimu mpya wa Ligi Kuu Bara, licha ya kutokuwa majeruhi wala kuwa na tatizo lolote, ila mwenyewe akafunguka na kutoa msimamo wake wa kurejesha namba kikosini.

Yanga imecheza mechi tatu mpaka sasa ikiongoza msimamo, lakini Mukoko licha ya kumaliza kutumikia adhabu yake ya kadi nyekundu aliyoipata kwenye fainali ya Kombe la Shirikisho (ASFC) dhidi ya Simba msimu uliopita na kuwa fiti, bado hajacheza msimu huu.

Akizungumza na gazeti la Mwanaspoti alisema anajua sababu ya kujikuta anakosa nafasi kuwa ni ubora wa timu ulivyo kwa sasa na huku timu ikizidi kuimarika ikishinda mechi zake.

Mukoko alisema anatambua ni vigumu kwa kocha wao Nesreddine Nabi kuanza kubadilisha sura ya kikosi kutokana na ubora ambao unaendelea kuonekana.

“Najua sababu. Wala sina tatizo kubwa katika hilo, mnakumbuka sikuwa naruhusiwa kucheza baada ya kusimamishwa, pia naona ubora wa timu kwa sasa upo juu, hii ni sababu na lazima nipambane,” alisema Mukoko ambaye ni nahodha msaidizi wa kikosi hicho.

“Namuelewa pia kocha (Nabi) ni vigumu kwake kubadilisha kikosi kwa sasa kwani timu inashinda, timu ikishinda sio tu wale wanaocheza sote tunafurahia, maana ndio malengo yetu na ndio sababu tuko hapa.”

Kiungo huyo aliyemaliza msimu uliopita na mabao matatu, alisema kutokana na ubora huo wa timu viungo wenzake waliopata nafasi Yannick Bangala na Khalid Aucho wamekuwa katika utulivu mkubwa.

“Wenzangu (Aucho na Bangala) nao wanacheza vizuri na wanaonekana kutulia na kutuliza timu, kwanza lazima uwapongeze kisha uwe na akili ya kujua utapataje nafasi mbele yao, hiki ndicho ninachokifanya sasa,” alisema Mukoko.

Alisema anajua bado nafasi yake ipo ndani ya kikosi hicho anachojipanga kuendelea kujiweka sawa na tayari ili siku akipata nafasi afanye kitu bora kama ambavyo alikuwa akifanya.

SOMA NA HII  MGANDA ALIYESAINI YANGA AKUTANA NA MTIHANI MZITO

“Mimi niko sawasawa sina tatizo kabisa, najiamini, siku zote natakiwa kuwa tayari, nafahamu nafasi yangu bado ipo.”