Home news KOCHA POLISI TANZANIA ACHEKELEA USAJILI WA METACHA MNATA

KOCHA POLISI TANZANIA ACHEKELEA USAJILI WA METACHA MNATA


 KOCHA Mkuu wa Polisi Tanzania, Malale Hamsini, ameweka wazi kuwa usajili bora wa vijana walioufanya akiwemo mlinda mlango, Metacha Mnata, ndiyo sababu ya kuwa na timu bora ambayo anaamini itawashangaza wengi msimu huu.

Metacha aliyesajiliwa na Polisi Tanzania baada ya kuachwa na Yanga, tayari amedaka katika mechi mbili za Polisi Tanzania na zote wameshinda.

Malale amesema kuwa kupata kwao ushindi kwenye mechi za mwanzo ni jambo ambalo wanahitaji kuona likiendelea hivyo watazidi kupambana kuwa imara.

 “Tunashukuru kwa kuanza msimu vizuri na kufanikiwa kushinda michezo miwili ya kwanza, kwangu haya ni matokeo ya kufanya usajili mzuri hasa wa vijana wadogo na wenye uwezo mkubwa kama kipa wetu Metacha Mnata.

“Kutokana na uwepo wa vijana wengi kwenye kikosi chetu, unaweza kuona timu imekuwa na kasi kubwa, ukiangalia mabao yote manne tuliyofunga katika michezo miwili iliyopita ilitokana na uwezo mkubwa wa kufanya mashambulizi ya kushitukiza, naamini kama tutaendelea hivi basi tunaweza kumaliza nafasi nzuri zaidi msimu huu.”

Mechi ya kwanza walishinda kwa mabao 2-0 dhidi ya KMC Uwanja wa Karatu na ule wa pili waliibuka wababe mbele ya Azam FC, Uwanja wa Ushirika Moshi kwa mabao 2-1.

SOMA NA HII  WAKIIVAA ASEC LEO...MASTAA SIMBA WATENGEWA MABILIONI..LWANGA AREJEA..NABI AFANYA UAMUZI MGUMU YANGA...