Home Ligi Kuu KOCHA POLISI TZ : SIMBA WAMESHINDA KWA KUBEBWA..ALIA PENALTI YA KIUJANJA UJANJA...

KOCHA POLISI TZ : SIMBA WAMESHINDA KWA KUBEBWA..ALIA PENALTI YA KIUJANJA UJANJA YA MORRIOSN..


Kocha Mkuu wa Polisi Tanzania FC Malale Hamsini amesema wapinzani wao Simba SC walibebwa dhahir katika mchezo wa juzi Jumatano (Oktoba 27).

Mchezo huo uliounguruma jijini Dar es salaam, Uwanja wa Benjamin Mkapa, ulishuhudia Simba SC ikipata bao la ushindi dakika ya 89 kwa njia ya penati iliyopigwa na Kiungo kutoka Zambia Rally Bwalya.

Mwamuzi aliamuru mkwaju huo kupigwa langoni mwa Polisi Tanzania, baada ya Kiungo kutoka nchini Ghana Bernard Morrison kuchezewa rafu eneo la hatari dakika ya 86.

Kocha Malale amesema maamuzi ya penati dhidi ya kikosi chake hayakua halali, hivyo anaamini Simba SC ilipata msaada wa ushindi kutoka kwa mwamuzi.

“Kikosi changu kimecheza vizuri na kupokea maelekezo yote tuliyowapa, ila kilichotuangusha ni maamuzi ya mwamuzi wa mchezo kwa kuizawadia Simba penati dakika ya (89′)”

“Hata zingeongezwa dakika ngapi Simba wasingepata bao dhidi ya vijana wangu ndio maana wakapewa penati na mwamuzi isiyo ya halali, penati waliyopewa ni ya ujanja ujanja kwa sababu Morrison aliufata mpira wa mguu kwa kichwa Kwa nini Mwamuzi atoe Penati” amesema Malale Hamsini.

Ushindi wa bao 1-0 umeipaisha Simba SC hadi nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwa kufikisha alama 7, huku Polisi Tanzania yenye alama 9 ikiporomoka kutoka nafasi ya kwanza hadi ya pili.

Young Africans inaongoza msimamo wa Ligi Kuu kwa kufikisha alama 9, baada ya kushuka dimbani mara tatu.

SOMA NA HII  KISA MDHAMINI MPYA SIMBA....VUNJA BEI AFUNGUKA KUPATA HASARA YA ML 349 KWENYE JEZI...AANIKA YOTE A-Z...