Home news KWA MARA NYINGINE TENA ..NIYONZIMA AFUNGUKA KUHUSU YANGA..ATOA ONYO KALI

KWA MARA NYINGINE TENA ..NIYONZIMA AFUNGUKA KUHUSU YANGA..ATOA ONYO KALI


NYOTA wa zamani wa Yanga, Haruna Niyonzima amekiri kikosi cha Yanga msimu huu kitakuwa tishio endapo wachezaji watapambana zaidi katika kila mchezo wanaokutana nao.

Niyonzima aliachana na Yanga baada ya kumaliza mkataba wake na kuagwa rasmi, kisha kutimkia AS Kigali ya nchini kwao Rwanda, huku akiendelea kuifuatilia timu yake hiyo ya zamani na kukiri kwamba mziki wao safari hii sio wa kitoto.

Alisema aina ya wachezaji waliopo kwa sasa ushindani ni mkubwa, hivyo uwezo wa kutwa taji la ligi wanao licha ya ushindani baina yao na watani zao Simba wanaolishikilia taji kwa misimu minne mfululizo.

SOMA NA HII  IKIWA LIGI NYINGI ZIMEISHAISHA..MERIDIANBET WANAKULETEA DILI HILI JIPYA LA KUCHOTA MAHELA...