Home Habari za michezo SINGIDA BIG STARS WAANZA KUONYESHA MAKUCHA YAO YA USAJILI…’WAMKWAPUA’ KIPA AZAM MCHANA...

SINGIDA BIG STARS WAANZA KUONYESHA MAKUCHA YAO YA USAJILI…’WAMKWAPUA’ KIPA AZAM MCHANA KWEUPEEE…


Aliyekuwa kipa wa Azam FC, Benedict Haule ‘Beko’ amesaini mkataba wa mwaka mmoja kuitumikia Singida Big Stars katika msimu ujao.

Beko amemaliza mkataba na Azam ndipo Uongozi wa Singida ukaona umuongeze katika kuimarisha eneo la kipa.

Usajili wa Beko kwenye kikosi hicho unaenda kuimarisha eneo la kipa kwani tayari alishasajiliwa Metacha Mnata kutoka Polisi Tanzania.

Akizungumzia usajili wake, Beko amesema ni jambo zuri kujiunga na timu huku akiweka wazi imani yake ni kufanya vizuri.

Beko amesema ana imani kubwa atakuwa sehemu ya wachezaji ambao wataisaidia timu hiyo kuwa miongoni mwa timu tishio.

“Mpaka nasajiliwa Uongozi umeona umuhimu wangu kuwa hapa, upande wangu sitowaangusha nitahakikisha naipambania timu,”amesema Beko.

Kipa huyo aliwahi kucheza katika timu za Mbao, Prisons na Azam FC kwa nyakati tofauti.

SOMA NA HII  KUTOKA SAUZI...BARBARA AFUNGUKA SABABU YA SIMBA KUKODI WALINZI WA AFRIKA KUSINI..