Home news TWIGA STARS KIBARUANI LEO KUWANIA KUFUZU AFCON WANAWAKE

TWIGA STARS KIBARUANI LEO KUWANIA KUFUZU AFCON WANAWAKE


Timu ya taifa ya Wanawake ‘Twiga Stars’ inataraji kushuka dimbani leo Oktoba 20, 2021 saa 10:00 jioni kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa kuikabili timu ya Namibia kuwania kufuzu michuano ya Afcon kwa Wanawake  mwaka 2022 nchini Morocco.

Mashindano hayo yanayotarajiwa kuanza Julai 2 hadi 23, 2022 nchini Morocco ambapo baada ya mchezo wa leo, Twiga  Stars watarejeana tena dimbani Oktoba 23, 2021 na mshindi wa jumla atapambana na mshindi kati ya Malawi na Zambia.

Mara ya mwisho kwa mataifa haya kukutana ilikuwa mwaka 2012 katika kutafuta nafasi ya kufuzu Afcon 2012  ambapo Namibia ilipoteza kwa jumla ya magoli 7-2 huku timu zote zikiwa zimewahi fuzu mara moja kwenye Afcon.

Twiga Stars ilifuzu Afcon mwaka 2010 kwa mara ya kwanza  ilhali Namibia walipata tiketi ya ushiriki mwaka 2014 kama muandaaji wa mashidano hayo.

SOMA NA HII  BAADA YA KUPONA.... DILUNGA AVUNJA UKIMYA SIMBA...KUMBE ERASTO NYONI NDIYE CHANZO....