Ligi Kuu

FT: SIMBA 1-0 NAMUNGO….KAGERE ATUPIA GOLI LA ‘KIALKASUSU’ …SASA NI MWENDO WA KIMYA KIMYA…

admin November 3, 2021 6:46 pm


Simba imevuna alama nyingine tatu kwenye Uwanja wa Mkapa baada ya kushinda bao 1-0 dhidi ya Namungo kwa bao liliwekwa wavuni na Meddie Kagere.

Kagere aliyeingia dakika za nyongeza alimalizia kwa kichwa krosi ya Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ na kumshinda mlinda mlango wa Namungo Jonathan Nahimana.

Katika mchezo huo Namungo, Simba walionekana kuendelea kusumbuliwa na kasumba ya kutumia nafasi ambazo wamekuwa wakitengeneza ikiwemo moja ya wazi aliyopoteza Kibu Denis.

Aliyekuwa akiongoza mashambulizi kwa wekundu hao wa msimbazi alikuwa ni mfungaji bora wa msimu uliopita, John Bocco kabla ya baadae kuingia Meddie Kagere.

Kagere ndiye aliyewapa raha mashabiki wa Simba mwishoni kabisa mwa kipindi cha pili, Mrwanda huyo alipachika bao lake la pili msimu huu na kuwanusuru mabingwa hao watetezi kuvutwa Shati na Namungo ambao walikuwa pungufu.

Namungo iliwabidi wamalize pungufu baada ya kiungo wao,  Abdulziz Makame kuonyeshwa kadi nyekundu kufuatia kumchezea vibaya, Shomari Kapombe dakika ya 54.

MAKOCHA YANGA WAVAMIA MECHI YA SIMBA vs NAMUNGO…NABI AJIFUNIKA NA KOFIA NYEUSI.. BAADA YA ‘KUWASHIKA HASWA’ YANGA…AUCHO ASHINDWA KUJIZUIA..UFUNGUKA KUHUSU DILI LAKE NA SIMBA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply