Home news KIMEELEWEKA…ISHU YA YANGA KUVAA NEMBO NYEUSI YA MDHAMINI..BODI YA LIGI WAJA NA...

KIMEELEWEKA…ISHU YA YANGA KUVAA NEMBO NYEUSI YA MDHAMINI..BODI YA LIGI WAJA NA HILI…


MKURUGENZI wa Bodi ya Ligi, Almasi Kasongo ametoa ufafanuzi kuhusu baadhi ya vilabu vya soka nchini kubadili nembo za wadhamini kwenye jezi zao.โ€œSuala la nembo ni suala la kikanuni na bodi ya ligi kazi yake kusimamia kanuni mwenye dhamana ya kusimamia hilo ni yule mwenye nembo yake.

โ€œBodi ya ligi inanembo yao TFF ina nembo yao na kila klabu ina nembo yake. Bodi tutasimamia kanuni zinavyosema na pia tutazingatia makubaliano baina ya mwenye nembo na klabu husika.

โ€œNa haiwezekani mwenye nembo aseme tumekubaliana na mhusika flani halafu bodi ipinge, bodi ipo kwa ajili ya kusave interest ya klabu na bodi ya ligi ni sulihisho na si kuwa chanzo cha tatizo kwa wadau wetu,โ€ CEO TPLB Almasi Kasongo akitolea ufafanuzi kwanini wamekubali Yanga SC kuvaa twiga mweusi.

SOMA NA HII  NYOTA WAWILI YANGA HATIHATI KUIKOSA MWADUI KISA UTOVU WA NIDHAMU