Home news HIVI NDIVYO YANGA ILIVYOIZIDI AKILI SIMBA KWA MSIMU HUU…MAKOCHA WAFUNGUKA..KAGERE AHUSISHWA…

HIVI NDIVYO YANGA ILIVYOIZIDI AKILI SIMBA KWA MSIMU HUU…MAKOCHA WAFUNGUKA..KAGERE AHUSISHWA…

 


YANGA ya msimu huu ni balaa, kwani rekodi zinaonyesha katika raundi tano za Ligi Kuu Bara, imewazidi ujanja watani, Simba kulinganisha na ilivyokuwa msimu uliopita katika idadi ya mechi kama hizo.

Katika mechi zao tano za awali za msimu huu, Yanga imekusanya pointi 15, nne zaidi na ilizonazo Simba, huku straika Meddie Kagere mwenye mabao mawili kwa sasa akishindwa kufikia moto aliokuwa nao msimu uliopita alipofunga mabao manne katika mechi kama hizo tano za awali.

Msimu uliopita Simba na Yanga kila moja ilikusanya pointi 13 baada ya kushinda mechi nne na kutoka sare mechi moja, huku Kagere akiingia mara nne kambani kwenye mechi tatu tofauti wakati msimu huu akiwa na mabao mawili tu.

Yanga msimu uliopita ilianza na sare ya bao 1-1 dhidi ya Tanzania Prisons, ikaibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mbeya City, 1-0 dhidi ya Kagera Sugar 1-0 na Mtibwa Sugar na ikamaliza na Coastal Union kwa kushinda mabao 3-0.

Wakati Simba ilianza na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Ihefu, sare ya 1-1 dhidi ya Mtibwa Sugar ushindi wa 4-0 dhidi ya Biashara United, ikaifumua Gwambina mabao 3-0 kisha kushinda tena 4-0 dhidi ya JKT Tanzania.

Simba michezo mitano ya kwanza msimu uliopita ilifunga mabao 14, huku Kagere akifunga matatu na msimu huu kwenye michezo mitano imefunga mabao matatu tu, huku Kagere akifunga mawili na Rally Bwalya, wakati Yanga ilifunga saba msimu uliopita na msimu huu imefunga mabao tisa. 

Michezo ya Yanga msimu huu ni dhidi ya Kagera Sugar 1-0, Geita Gold 1-0, ikaichapa KMC kwa mabao 2-0 kama ilivyofanya kwa Azam FC kisha kuizamisha Ruvu Shooting kwa mabao 3-1 na kukusana pointi 15, huku watani wao wakianza na suluhu dhidi ya Biashara Utd na Coastal Union, ikazichapa kwa bao 1-0 timu za Dodoma Jiji, Polisi Tanzania na Namungo na kukusanya alama 11 na mabao manne ya kufunga na kutofungwa bao hata moja hadi sasa.

SOMA NA HII  BEKI WA WYDAD AMUIGA MAYELE...LIGI YA MABINGWA AFRIKA...ISHU NZIMA IKO HIVI

MAKOCHA WAFUNGUKA

Kocha wa zamani wa Simba, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ alisema ni mapema sana kutabiri nani ni bora zaidi ya mwenzake japo wapinzani wanaonekana kuwa na kikosi bora ila kama Simba watatumia vizuri mapumziko na kutafuta haraka kocha mkuu wa kuiongoza timu wanaweza kurudi vizuri.

“Kuna makosa madogo madogo kwa Simba wanajisahau na kujiamini sana hawajui kama msimu huu ni wa ushindani kila timu imejipanga kufanya vizuri hii ni kutokana na pesa nyingi iliyowekwa na Azam kila mmoja ashinde mechio zake hivyo kwasasa sitaki kuzungumza sana kuhusu hizi timu mbili hazitabiriki,” alisema.

Kocha wa Biashara, Patrick Odhiambo alisema “Simba ni wazuri na wanawachezaji wapambanaji shida haijajulikana ni nini kama wanahitaji matokeo na kuona timu yao inafanya vizuri wanatakiwa kukaa na wachezaji wawaulishe nini kinawafanya washindwe kufanya vizuri,” alisema na kuongeza kuwa;

“Kwa upande wa Yanga ni bora kila eneo wametafuta jeshi kubwa la ushindani kila mchezaji anaubora wake na kuna wenye uzoefu mkubwa na mashindano ukiachana na ligi kuu bara,” alisema

Naye Mohammed ‘Adolf’ Rishard alisema Simba inacheza vizuri na inatengeneza nafasi lakini inakosa umakini ikifika ndani ya 18 wanahitaji kuongeza umakini ili kuweza kufikia mafanikio ni mapema sana kuwasema mabaya yao kwani hata msimu uliopita walikuwa hivyo japo msimu huu wamepunguza ubora hasa ushambuliaji.

“Yanga washindwe wao tu kwani kwa upande wa viongozi wamekamilisha kila kitu wanachosubiri ni matokeo kutoka kwa wachezaji lakini kuanzia benchi la ufundi na wachezaji ni bora,” alisema.