Habari za michezo
HUU HAPA UKWELI WOTE KUHUSU ‘MOVE’ YA MANULA KWENDA AZAM KIRAHISI RAHISI….
HUKU ikitaja sababu tatu za kumrejesha golikipa, Aishi Manula kundini baada ya kumpoteza kwa kipindi cha miaka minane, uongozi wa Azam FC, umesema ujio wa Aishi Manula katika klabu hiyo ni pendekezo la Kocha Mkuu Florent Ibenge.
Klabu hiyo ilimtangaza rasmi kuwa mchezaji wao juzi, ingawa hili lilianza kufahamika kuwakipa huyo kutimkia Azam tangu Juni 11, mwaka huu.
Manula alijiunga na Simba mwaka 2017, akiwa na wachezaji wenzake, Shomari Kapombe, Erasto Nyoni na John Bocco, ambapo kati ya hao wote ni Kapombe tu ambaye amesalia.
Akizungumza jijini Dar es Salaam Jana, Ofisa Habari wa Klabu hiyo Thabit Zakaria maarufu Zaka Zakazi, alisema Kocha huyo alimpendekeza mlinda mlango huyo kutokana na kutambua thamani yake.
“Tusingeweza kumsajili Manula bila kuzungumza na kocha, ameridhia ndio maana tukamjumuisha kwenye kikosi chetu,” alisema Zaka Zakazi.