news

KISA UBINGWA LIGI KUU…YANGA WATANGAZA HALI YA HATARI…

admin November 12, 2021 5:10 am

 


UONGOZI wa klabu ya Yanga umetamba kuwa moto walioanza nao kwenye Ligi Kuu Bara msimu huu hauzimiki, bali wataendelea kukusanya pointi tatu katika kila mchezo ulio mbele yao ili kutimiza jambo lao la kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu huu.

Yanga wameanza vizuri msimu huu ambapo mpaka sasa kwenye Ligi Kuu ndio vinara wa msimamo, wakiwa wamejikusanyia pointi 15 baada ya kuibuka na ushindi katika michezo yao mitano waliyocheza.

Mchezo ujao wa Yanga ni wa ugenini dhidi ya Namungo utakaopigwa Novemba 20, mwaka huu kwenye Uwanja wa Ilulu mkoani Lindi.

Akizungumza hivi karibuni Ofisa habari wa klabu ya Yanga, Hassan Bumbuli alisema: “Kwetu sisi nguvu kubwa tumewekeza katika timu yetu kuhakikisha tunafanya vizuri katika kila mchezo ulio mbele yetu ili kufanikisha dhumuni la kushinda ubingwa wa Ligi Kuu msimu huu.

“Tunajua ligi ya msimu huu ni ngumu, lakini tunajivunia ubora wa kikosi tulichonacho ambao kwa kiasi kikubwa tuna uhakika kinaweza kutimiza malengo tuliyojiwekea.”

KUHUSU KOCHA MPYA WA SIMBA..YANGA WASHINDWA KUJIZUIA…INJINIA HERSI AFUNGUKA HAYA… MKATABA WA KOCHA MPYA SIMBA NI KUFURU YA FUNGA MWAKA…KILA KOMBE AKISHINDA ANALIPWA MAMILIONI..

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply