Home news HITIMANA: UJIO WA KOCHA MPYA HAUNA FAIDA KWA WACHEZAJI….MABADILIKO YATAANZA…

HITIMANA: UJIO WA KOCHA MPYA HAUNA FAIDA KWA WACHEZAJI….MABADILIKO YATAANZA…


Kocha Msaidizi wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC, Thierry Hitimana amesema mazoezi ya Bosi wake Kocha Franco Pablo Martin yamekua na faida kubwa kwa kila mmoja klabuni hapo.

Hitimana ambaye alikaimu nafasi ya Kocha Mkuu kwa majuma mawili baada ya kuondoka kwa Mfaransa Didier Gomes amesema si wachezaji tu wananufaika na mbinu za kocha huyo kutoka nchini Hispania, bali hata yeye kuna vitu vingi vipya ameanza kujifunza.

Hitimana amesema kuna mambo mengi mapya anayapata kutoka kwa kocha Franco na anaamini ni muda tu unahitajika kabla ya mashabiki kushuhudia mabadiliko makubwa katika kikosi chao.

“Ujio wa Kocha mpya hauna faida kwa wachezaji pekee yake, bali hata mimi kuna baadhi ya mambo ninaendelea kujifunza, ninaamini mabadiliko yataanza kuonekana muda si mrefu.” amesema Kocha Hitimana.

Kocha Franco Pablo Martin alianza kukinoa kikosi chake mwishoni mwa juma lililopita, baada ya kuwasili jijini Dar es salaam siku ya Alhamis (Novemba 11) akitokea nchini kwao Hispania.

SOMA NA HII  JOB:- MAMELOD WAMESHAJAA KWENYE MFUMO....5G ITAHUSIKA TU....