News

AJIBU YAMKUTA SIMBA…PABLO AMUONDOA KIKOSINI MAPEMA TU…ISHU NZIMA IKO HIVI….

admin November 19, 2021 12:02 pm

 


KOCHA Mkuu wa Simba, Mhispania, Pablo Franco, amemuondoa kiungo mshambuliaji wa timu hiyo,Ibrahim Ajibu katika mipango yake.

Hiyo ni katika kuelekea mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Ruvu Shooting ambao utapigwa leo Ijumaa saa 10:00 jioni kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.

Pablo, huo utakuwa mchezo wake wa kwanza wa mashindano kukaa kwenye benchi akiiongoza timu hiyo akisaidiana na wasaidizi wake, Thiery Hitimana na Selemani Matola.

Mwenyekiti wa timu hiyo, Murtaza Mangungu ameliambia Championi Ijumaa kuwa kiungo huyo atakosekana katika mchezo huo baada ya kupata majeraha katika mazoezi ya mwisho ya timu hiyo.

Mangungu alisema kuwa kiungo huyo alijikwaa uwanjani akifanya mazoezi kwenye Uwanja wa Boko Beach Veterani jijini Dar es Salaam.

“Ajibu hatakuwepo katika sehemu ya kikosi kitakachocheza dhidi ya Ruvu kesho (leo) kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.

“Ni baada ya kupata majeraha mazoezini, alijikwaa mguuni akiwa anakimbia na kusababisha kupata maumivu,” alisema Mangungu.

PABLO AWATAJA MASTAA WATATU WA MAANA SIMBA…KISUBI, ABDULSWAMAD KUONDOLEWA…. KAGERE, KIBU DENIS KUONGOZA MASHAMBULIZI DHIDI YA RUVU SHOOTING…KIKOSI KAMILI HIKI HAPA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply