News

KAGERE, MKUDE NA MORRISON KUCHUANA TUZO YA MCHEZAJI BORA SIMBA…

admin November 29, 2021 5:00 pm


Nyota  watatu wa Simba SC Bernard Morrison, Jonas Mkude na Medie Kagere wameingia fainali ya kinyang’anyiro cha Mchezaji Bora wa Mashabiki wa Novemba (Emirate Aluminium ACP Simba Fans Player of the Month).

Kuchaguliwa kwa wachezaji hao kumetokana na uwezo mkubwa walioonyesha katika mechi tulizocheza Novemba.

Awali walikuwa wachezaji watano akiwamo walinzi Joash Onyango na Mohamed Hussein lakini wamechujwa na Kamati Maalumu na kubaki watatu ambao watakaopigiwa kura na mashabiki.

Zoezi la kupiga kura limefunguliwa leo na litafungwa Desemba Mosi saa 10 jioni ambapo atakayepata kura nyingi atatangazwa mshindi.

Hassan Dilunga aliibuka mshindi wa mwezi Oktoba na kujinyakulia kitita cha Sh 2,000,000 kutoka kwa wadhamini wa tuzo Emirate Aluminium ACP.

MWAMUZI ALIYEWAPA YANGA PENATI YA UTATA DHIDI YA NAMUNGO..AKIONA CHA ‘MTEMA KUNI’… PAMOJA NA USHINDI WA GOLI 3-0, PABLO ASHINDWA KUJIZUIA..AWACHANA WACHEZAJI SIMBA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply