News

DAKIKA CHACHE KABLA YA SIMBA vs YANGA..IBENGE AFUMBA MACHO AIPA USHINID TIMU HII….

admin December 11, 2021 1:14 pm


KOCHA Mkuu wa RS Berkane ya Morocco, Florent Ibenge, ameitabiria Yanga kuondoka na ushindi mbele ya Simba katika mchezo wa dabi ya Kariakoo utakaochezwa leo Jumamosi katika Uwanja wa Mkapa,Dar.

Ibenge ambaye aliwahi kuwa Kocha Mkuu wa AS Vita na timu ya taifa ya DR Congo, analifahamu vyema soka la Tanzania akiwa amewahi kukutana na Simba na Taifa Stars.

Kocha huyo ndiye anayewafundisha viungo wa zamani wa timu hizo, Clatous Chama na Tuisila Kisinda.

Ibenge aliliambia Championi Jumamosi kuwa anauona mchezo ukiwa mgumu kwa timu zote huku akiipa nafasi Yanga ya kuibuka na ushindi kutokana na kuwa na mwanzo mzuri wa ligi pamoja na kufanya usajili mzuri ambao umewasaidia kuwa bora.

“Mchezo utakuwa mgumu kwa kuwa ni mchezo wa dabi. Simba nimekutana nao mara kwa mara nikiwa na AS Vita, mara zote nimewaona wakiwa bora lakini kwa sasa hawapo vizuri sana, kuna kitu kimepungua kwao, jambo ambalo naamini litakuwa faida kwa Yanga.

“Yanga wameanza vizuri katika ligi, usajili ambao wameufanya umekuwa bora kwao na umewafanya kuonekana katika muundo mzuri wa timu wakiwa na faida ya maelewano ya haraka, hivyo kama watafanikiwa kuwa katika ubora wao naamini watapata ushindi mbele ya Simba,” alisema Ibenge.

KUELEKEA KARIAKOO DABI…VIKOSI VYA TIMU ZOTE HIVI HAPA…MORRISON KAMA KAWA KULIANZISHA… DAKIKA KADHAA KABLA YA KARIAKOO DABI…BARBARA AIBUKA NA JIPYA KUHUSU MORRISON NA MKUDE…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply